Thursday, May 16, 2013

MLIPUKO WA BOMU BAGHDAD - 5 WAUAWA NA 19 WAJERUHIWA.

Mripuko wa bomu la kutegeshwa kwenye gari katika mji wa Baghdad umewauwa kiasi ya raia watano.Maafisa wawili wa polisi wamesema gari hilo lililokuwa limewekwa viripuko liligonga basi na  kituo cha texi leo asubuhi wakati watu wengi wakiwa katika pirika pirika mjini Sadr.

Mripuko huo pia uliwajeruhi watu 19.Afisa wa afya katika hospitali iliyo karibu na mkasa huo amethibitisha idadi ya waathiriwa.Shambulio la leo linakuja siku moja baada ya wimbi la mashambulio hapo jana ambayo yaliwauwa watu 33 katika mitaa inayokaliwa na washia.

Mashambulio hayo yanaongezeka wakati kuna hali ya wasiwasi kati ya serikali inayoongozwa na washia na wasunni walio wachache wanaohisi wanazingatiwa kama raia wa daraja la pili.

Source:DW

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...