Thursday, May 16, 2013

MAREKANI YATOA USHAHIDI KUHUSU TUKIO LA SHAMBULIZI LA BENGHAZI- LIBYA.

Ikulu ya White House imetoa mamia ya barua pepe na kumbukumbu kuhusu majibu ya utawala wa Obama kwa mashambulizi yaliyofanyika katika ubalozi wa Marekani huko Benghazi Libya, Septemba ilopita.
Katika tukio hilo aliyekuwa balozi wa Marekani nchini humo, Chris Stevens na watu wengine watatu waliuawa.
Wanachama wa Republican wamekuwa wakiulaumu utawala wa Obama kuhusiana na majibu yake.
Mwandishi wa BBC huko Washington anasema kuwa Ikulu ya White House iliamua kutoa stakabadhi hizo kuunga mkono msimamo wao kuwa wanachama wa Republican wamekuwa wakitumia tukio hilo kuleta matatizo.
Serikali ya Obama, ilitoa barua pepe hizo Jumanne katika hatua yake ya kutaka kuzima ukosajai kutoka kwa wapinzani wao.
Hadi sasa Ikulu ilikuwa imekataa kuzitoa huku jukumu la kuzinchunguza na kuzikagiua ikiachiwa wachunguzi wa Congress bila ya kuzipiga chapa.
Barua pepe hizo zenye kurasa 99 pamoja na ujumbe mwingine ulioandikwa kwa mkono, ukiwa wa mawasiliano kati ya majasusi wa CIA na FBI.
Katika barua hizo, inaonekana majasusi wa CIA, walikuwa katika msitari wa mbele katika mashauriano hayo na hata kukosa kutoa maelezo kuhusu tisho la kutokea mashambulizi. .
Inaarifiwa taarifa muhimu haikujumuishwa kwenye mashauriano hayo kulingana na stakabadhi, baada ya majasusi wa CIA kuhoji taarifa za kijasusi kuhusu nani aliyehusika na vifo vya maafisa wa Marekani.
Siku tano baada ya shambulizi hilo, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa, Susan Rice, alitumia baadhi ya stakabadhi na kusema kuwa mashambulizi yalitokea ghafla kutokana na maandamanao yaliyokuwa yanafanywa dhidi ya Marekani baada ya kuundwa filamu nchini humo ya kumkejeli Mtume Mohammed.
Siku ya Jumatano, msemaji wa Ikulu ya White House, Eric Schultz, alisema kuwa barua pepe hizo ni ushahidi wa kilichotokea na zitasaidia wanachunguzi wa kesi hiyo.

Source:BBC

No comments:

Post a Comment

LinkWithin

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...